TIMU ya Argentina imepangwa pamoja na Uruguay katika Kundi B kwenye michuano ya Copa America mwakani, 2015.
Droo hiyo pia imezikutanisha Colombia na wenyeji wa Kombe la Dunia 2014, Brazil. Michuano hiyo itakayofanyika nchini Chile, itashuhudia timu hizo mbili za Amerika Kusini zikikutana tena kwa mara nyingine, baada ya kukutana mara mbili hivi karibuni.
Brazil iliitoa Colombia katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia Julai, kabla ya Neymar kufunga bao la ushindi katika mechi ya kirafiki baina ya mataifa hayo mawili Septemba.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi ataiongoza Argentina kwenye Copa America ambako wamepangwa pamoja na Chile
Rais wa Chile, Michelle Bachelet akiwa ameshika taji la Copa America (kushoto), wakati Rais wa Shirikisho la Soka Uruguay (AUF), Valdez akiliwasilisha Kombe hilo wakati upangwaji wa droo
0 comments:
Post a Comment