MANCHESTER City imeshinda mabao 3-2 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.
Sergio Aguero alifunga mabao mawili dakika za mwishoni ili kuipatia ushindinhuo Manchester City, ambao sasa wanafufua matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano ya michuani hiyo.
Aguero aliifungia bao la kuongoza City dakika ya 21 kwa penalti iliyomponza Mehdi Benatia kutolewa kwa kadi nyekundu kwa rafu aliyocheza.
Bayern Munich ikatoka nyuma na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Xabi Alonso dakika ya 40 na Robert Lewandowski dakika ya 45.
Lakini shukrani kwake Aguero aliyeifungia City dakika ya 85 na 90 kukamilisha hat trick yake jana.
City sasa itasafiri kuwafuata Roma kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kundi hilo Jumatano ya Desemba 10 ikihitaji ushindi ili ifuzu.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Sagna/Zabaleta dk68, Kompany, Mangala, Clichy, Fernando, Milner/Jovetic dk66, Jesus Navas, Lampard, Nasri na Aguero/Demichelis dk94.
Bayern Munich; Neuer, Rafinha, Benatia, Boateng, Bernat, Alonso, Hojbjerg, Rode/Dante dk25, Robben, Lewandowski/Shaqiri dk84 na Ribery/Schweinsteiger dk81.
Sergio Aguero akikimbia kushangilia baada ya kuifungia hat-trick Man City jana dgudi ya Bayern Munich
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2848858/Manchester-City-3-2-Bayern-Munich-Sergio-Aguero-hits-stunning-late-double-rescue-Manuel-Pellegrini-s-complete-remarkable-hat-trick.html#ixzz3K8lfBWOe
0 comments:
Post a Comment