GWIJI Zinedine Zidane amesimamishwa kufundisha soka kwa miezi mitatu katokana na kutokuwa hadhi ya kiwango cha tatu, Level 3 kwa mujibu wa Mamlaka za Hispania.
Mshindi huyo wa zamani wa Kombe la Dunia, awali alikuwa Msaidizi wa Carlo Ancelotti katika timu ya kwanza ya Real Madrid mwaka 2013 kabla ya kupelekwa kuwa kocha wa timu ya pili, Castilla B, huku Msaidizi wake, Santiago Sanchez akitajwa kuwa kocha mkuu.
Pamoja na hayo, kufuatia malalamiko yasiyo rasmi, yaliyowasilishwa Shirikisho la Soka Hispania, Jaji wa Daraja la Segunda B, Francisco Rubio ameamua kuwafungia Zidane na Sanchez kufundisha kwa miezi mitatu.
Nyota huyo wa zamani wa Madrid ana leseni A ya UEFA, inayotokana na had hi ya kiwango cha pili, Level 2. Amenusurika kufungiwa miezi sita na sasa anatakiwa kwenda kusomea Level 3 ya ukocha wake Ufaransa hadi kufika Aprili 2015.
Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 42 sasa, awali alilalamikia namna ambavyo anafanyiwa katika sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment