Na Samira Said, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya Yanga SC leo asubuhi kimeondoka jijini Dar es Salaam na kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kucheza mechi moja ya ‘ndondo’ dhidi ya timu ya CDA ya mkoani humo.
Mechi hiyo kati ya CDA ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili ya mkoa dhidi ya Yanga inatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Kikosi cha Yanga kimeondoka leo asubuhi kikiwa na wachezaji wake wote na kimetumia usafiri wa basi lao ambalo walipewa na wadhamini wa klabu hiyom Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager.
Baada ya mechi hiyo ya kirafiki, Yanga itaelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kwenda kuwakabili wenyeji, Stand United katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itakayofanyika Jumamosi Oktoba 25 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Yanga itaendelea kukaa Kanda ya Ziwa kwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki mjini Kahama na baadaye kuelekea Bukoba mkoani Kagera kuwavaa Kagera Sugar katika mechi ya ligi itakayochezwa Novemba Mosi kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Kikosi cha Yanga SC kitaweka kambi Dodoma kabla kwenda Shinyanga |
Baada ya mechi hiyo ya kirafiki, Yanga itaelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kwenda kuwakabili wenyeji, Stand United katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itakayofanyika Jumamosi Oktoba 25 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Yanga itaendelea kukaa Kanda ya Ziwa kwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki mjini Kahama na baadaye kuelekea Bukoba mkoani Kagera kuwavaa Kagera Sugar katika mechi ya ligi itakayochezwa Novemba Mosi kwenye Uwanja wa Kaitaba.
0 comments:
Post a Comment