Na Asha Said, DAR ES SALAAM
VILLA Squad imelazimisha sare ya bila kufungana na Friends Rangers ‘Wakombozi wa Manzese’ katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jioni ya leo.
Timu hizo za Dar es Salaam ziliumana vikali leo katika mchezo huo uliokuwa wa kupaniana na matokeo yake, dakika 90 zikamalizika kwa sare hiyo tasa.
Matokeo hayo, yanaifanya Rangers inayofundishwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yussuf ‘Tigana’ itimize pointi nane, baada ya mechi nne, ikishinda mbili na kutoa sare mbili.
Villa Squad yenyewe ambayo imewahi kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara mbili ndani ya muongo huu, inakuwa na pointi mbili baada ya kufungwa mara mbili na kutoa sare mbili.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, JKT Oljoro imepata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Warriors.

Friends Rangers wamepunguzwa kasi na Villa Squad safari la Ligi Kuu leo Karume |
Villa Squad yenyewe ambayo imewahi kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara mbili ndani ya muongo huu, inakuwa na pointi mbili baada ya kufungwa mara mbili na kutoa sare mbili.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, JKT Oljoro imepata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Warriors.
0 comments:
Post a Comment