KIPA Victor Valdes leo amefanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Manchester United viwanja vya Carrington tayari kukamilisha usajili wa kushitukiza Old Trafford ndani ya wiki mbili.
Gwiji huyo na kipa wa zamani wa Barcelona, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, yuko kwenye mazungumzo na kocha wa United, Louis van Gaal.
Wakala wa Valdes, Gines Carvajal na wawakilishi wengine wamekutana na viongozi wa United, na Van Gaal kuangalia uwezekano wa kukamilisha usajili huo ndani ya wiki mbili.
Kipa huyo aliyecheza Barcelona tangu 2002 hadi 2014, akicheza jumla ya mechi 535- pia ameichezea timu ya taifa ya Hispania tangu mwaka 2010 jumla ya mechi 20.
Valdes anashikilia rekodi ya kipa aliyesimama langoni muda mrefu bila kufungwa akiwa Barcelona - dakika 896.
Mchezaji mpya wa Manchester United, Ander Herrera, ndiye aliyevunja rekidi hiyo wakati anacheza Athletic Bilbao, baada ya kumfunga Valdes.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32, ameshinda tuzo ya Zamora ambayo inamaanisha kipa bora wa La Liga mara tano na pia anashikilia rekodi ya kipa aliyedaka mechi nyingi zaidi Barcelona. Kwa sasa, matatizo yake ya goti yanachunguzwa na United.
Valdes akiwa ameinua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Barcelona kuifunga Man United katika fainali mwaka 2009 mjini Rome, Italia.
0 comments:
Post a Comment