BARCELONA imetwaa taji la Super Cup la Katalunya kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Espanyol, baada ya sare ya 1-1 usiku wa jana.
Luis Suarez alimsetia Gerard Pique kuifungia Barca bao la kuongoza dakika ya 16, kabla ya Espanyol kusawazisha mjini Girona kupitia kwa Anaitz Arbilla, aliyepiga shuti zuri la mpira wa adhabu dakika ya 51.
Barcelona wakifurahia na taji lao usiku wa jana |
Katika mikwaju ya penalti Xavi, Halilovic, Grimaldo na Rakitic waliifungia Barca, huku Sandro akikosa, wakati upande wa Espanyol Victor Sanchez na Jordan pekee ndiyo waliofunga, huku Arbilla na Abraham wakikosa.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Masip, Adriano/Grimaldo dk73, Pique/Ie dk46, Bartra, Alba/Alba dk46, Samper/Halilovic dk75, Sergi Roberto/Xavi dk61, Rafinha/Rakitic dk61, Munir, Suarez/Adama dk46 na Pedro/Sandro dk46.
Espanyol: Pau, Mattioni/Victor Sanchez dk46, Raul Rodriguez, Victor Alvarez/Joan Jordan dk46, Salva Sevilla/Abraham dk46, Alex/Luque dk46, Clerc/Duarte dk46, Arbilla, Jairo, Bailly, Pol Llonch/Mamadou dk46.
Suarez sasa amefikisha pasi mbili za mabao katika mechi mbili alizozichezea Barcelona, kuanzia mechi dhidi ya Real Madrid Jumamosi
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2813279/Barcelona-1-1-Espanyol-4-2-pens-Luis-Suarez-produces-superb-lobbed-assist-Gerard-Pique.html#ixzz3HbHXjDHU
0 comments:
Post a Comment