// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC SARE TENA 1-1, PRISONS WACHOMOA DAKIKA YA MWISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC SARE TENA 1-1, PRISONS WACHOMOA DAKIKA YA MWISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, October 25, 2014

    SIMBA SC SARE TENA 1-1, PRISONS WACHOMOA DAKIKA YA MWISHO

    Na Renatus Mahima, MBEYA
    SIMBA SC imetoa sare ya tano mfululizo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Prisons jioni hii Uwanja wa Sokoine mjini hapa. 
    Simba SC ilikaribia kabisa kuondoka na ushindi katika mchezo huo, lakini makosa yaliyotokana na uzoefu mdogo wa kipa Peter Manyika, yaliizawadia bao jepesi la kusawazisha Prisons dakika ya 89.
    Manyika alianguka akalala kwenye boksi, refa akamuambia inuka- wakati huo mchezo unaendelea, naye akainuka na wakati anarudi kangoni, Hamisi Maingo akapiga shuti langoni la kufunga.

    Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya nane kwa shuti la mpira wa adhabu, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Jumanne Elfadhil.dk78 kipind cha pili pas javu 
    Simba SC inaokota pointi ya tano katika mechi tano na sasa inaelekea katika mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar wiki ijayo.
    Kikosi cha Prisons kilikuwa; Mohammed Yussuf, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, Lugano Mwangama, James Mwasote, Jumanne Elfadhil, Jeremiah Juma, Freddy Chudu, Ibrahim Hassan, Amir Omar na Lambert Sabianka. 
    Simba SC; Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla/Amri Kiemba dk58, Elius Maguli, Amisi Tambwe na Emmanuel Okwi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC SARE TENA 1-1, PRISONS WACHOMOA DAKIKA YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top