SHABIKI jana lilivamia uwanjani na kutaka kumshambulia nyota wa Bayern Munich, Franck Ribery, lakini likaishia kumtupia skafu usoni baada ya kudhibitiwa na Polisi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mchezo huo, ambao Bayern Munich ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Hamburg katika Raundi ya Pili ya Kombe la Ujerumani usiku wa jana.
Imekuwa kawaida ya mashabiki wa Hamburg kumzomea Robery kila anapokutana nao na jamaa huyo alivamia uwanjani na kwenda kumtupia winga huyo Mfaransa skafu huyo.
Mabao ya Bayern ambayo mechi ijayo itakutana na Borussia Dortmund katika Bundesliga, yalifungwa na David Alaba, Robert Lewandowski na Ribery.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2813352/Franck-Ribery-hit-face-pitch-invader-s-scarf-Bayern-Munich-s-German-Cup-victory-Hamburg.html#ixzz3HbLvPimG
0 comments:
Post a Comment