NAHODHA Wayne Rooney yuko fiti kucheza mechi ya wapinzani wa Jiji la Manchester mwishoni mwa wiki.
Rooney alizua hofu United Jumatatu, wakati alipotolewa nje mazoezini viwanja vya Carrington.
Pamoja na hayo, Nahodha huyo wa United, alifanya mazoezi kikamilifu jana na atacheza dhidi ya Man City Uwanja wa Etihad.
Rooney atarejea katika mechi ya mahasimu wa Manchester baada ya kumaliza adhabu ya mechi tatu
Rooney hajacheza tangu mwezi uliopita baada ya kutumikia adhabu ya mechi tatu kufuatia kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya West Ham.
Kocha wa United, Louis van Gaal amemuambia Rooney wazi ataanza katika mchezo huo, maana yake Robin van Persie ndiye anaweza kuanzia benchi licha ya kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Chelsea Uwanja wa Old Trafford Jumapili.
0 comments:
Post a Comment