NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa tena tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kumpiku mpinzani wake, Lionel Messi katika tuzo za Ligi ya Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa La Liga usiku wa Jumatatu baada ya kuwafungia mabao 31 katika ligi mabingwa hao wa Ulaya.
Hilo linaweza kuwa pigo kwa Messi, ambaye alitwaa kila tuzo miaka mitano iliyotangulia.
Cristiano Ronaldo (kushoto), akiwa na mpenzi wake Irina Shayk wakati wa kupokea tuzo hizo
TUZO ZA LIGA
Mchezaji Bora: Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Kocha Bora: Diego Simeone - Atletico Madrid
Kipa Bora: Keylor Navas - Real Madrid (zamani Levante)
Beki Bora: Sergio Ramos - Real Madrid
Kiungo Bora wa ulinzi: Luka Modric - Real Madrid
Kiungo Bora mshambuliaji: Andres Iniesta - Barcelona
Mshambuliaji Bora: Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Mchezaji Bora wa Afrika: Yacine Brahimi - Granada
Mchezaji Bora wa Amerika Kusini: Carlos Bacca - Sevilla
Mchezaji Bora Chipukizi: Rafinha Alcantara - Barcelona (mkopo Celta 2013-14)
Bao Bora: Cristiano Ronaldo (vs Valencia) - Real Madrid
Mchezo wa Kiungwana: Ivan Rakitic - Barcelona (zamani Sevilla)
Ronaldo ametwaa pia tuzo ya bao bora la msimu alilofunga dhidi ya Valencia hapa
0 comments:
Post a Comment