KLABU ya Chelsea itakutana na Derby County katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi, wakati Newcastle itapambana na Tottenham baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, na mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City usiku wa jana.
Timu ya Alan Pardew imetinga Robo Fainali baada ya mabao ya Rolando Aarons na Moussa Sissoko kuwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya City, ambayo jana imetimiza mechi tatu bila ushindi.
timu ya Eddie Howe, FC Bournemouth yenyewe imepewa vigogo wengine wa England, Liverpool na watasafiri hadi Pwani ya Kusini.
Timu hizo mbili zinafahamiana vyema baada ya mwaka jana kukutana katika Kombe la FA, wakati Derby - ambayo iliitoa Fulham Uwanja wa Craven Cottage Jumanne itaikaribisha Chelsea huko Midlands.
Kocha wa Chelsea, Jose Marounho amepania kutwaa mataji yote England msimu huu na bila shaka kuanzia hatua hii ya Capital One Cup atahitaji kutumia wachezaji wake bora ili kupata matokeo mazuri.
Mechi hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi ujao, Desemba 15.
0 comments:
Post a Comment