// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 23, 2014

    RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
    Hafla ya ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.
    Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
    Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
    Meneja wa Azam FC, Jemadari Said kulia naye ameshiriki kozi hiyo ya CAF

    Pia wapo Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yussuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
    Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top