KIUNGO David Silva hatacheza keshokutwa mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester katokana na maumivu ya goti.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kiungo huyo wa Hispania atakuwa nje kwa wiki tatu au nne baada ya kuumia goti lake Jumatano usiku katika mchezo wa Kombe la Ligi, England maarufu kama Capital One Cup.
Man City ilifungwa 2-0 na kutolewa na Newcastle United, iliyotinga Robo Fainali.
Silva hataukosa mchezo huo wa Jumapili wa Ligi Kuu ya England dhidi ya mahasimu Man United pekee, bali atakosa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo na CSKA Moscow Uwanja wa Etihad.
0 comments:
Post a Comment