KLABU ya Chelsea imetangaza kwamba Ron Gourlay anaachia wadhifa wake wa Mtendaji Mkuu na mwanamke, Marina Granovskaia anatarajiwa kumrithi.
Mscotland huyo, aliyejiunga na klabu mwaka 2004 na kuanza kazi kama Ofisa Mwendeshaji Mkuu kabla ya kurithi mikoba ya Peter Kenyon ya Utendaji Mkuu mwaka 2009, anaondoka ili kwenda kutafuta fursa nyingine.
Marina Granovskaia, mmoja wa washauri wa Roman Abramovich, ndiye aliyefanikisha usajili wa Diego Costa na pia kurejea kwa kocha Jose Mourinho Chelsea- na sasa anajiandaa kupewa majukumu makubwa zaidi Stamford Bridge.
HABARI ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2803380/chelsea-announce-ron-gourlay-leave-role-chief-executive-10-years-club.html#ixzz3Gup7QfxM
0 comments:
Post a Comment