KOCHA David Moyes yumo kwenye orodha fupi ya mwisho ya makocha wanaotakiwa na Inter Milan ya Italia inayotaka kumtimua kocha wake wa sasa, Walter Mazzarri.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United na Everton anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Mazzarri, ambaye timu yake inacheza na Cesena leo akiwa katika shinikizo baada ya mwanzo mbaya unaoifanya Inter iwe katika nafasi ya tisa kwenye msiamo wa ligi hivi sasa.
Moyes mwenyewe amekua akiamini akipata nafasi ya kufundisha klabu nje ya Uingereza itakuwa ni fursa nzuri kwake kurejesha heshima yake- hivyo akifanikiwa mpango huo atakuwa ametimiza ndoto zake kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment