Kocha Joseph Marius Omog (kushoto) amefungwa mecbhi ya kwanza Ligi Kuu jana tangu aanze kazi Desemba mwaka jana
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
REKODI ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kucheza mechi 18 za Ligi Kuu ya Voacom Tanzania Bara tangu ajiunge na Azam FC Desemba mwaka jana bila kufungwa, imevunjwa jana.
Omog aliajiriwa kwa pamoja na Mcroatia Zdravko Logarusic kwa upande wa Simba SC na Mholanzi Hans van der Pluijm, lakini wataalamu wenzake hao wote tayari wameondolewa baada ya kumalizia nusu ya msimu uliopita wa Ligi Kuu.
Azam ilifungwa 1-0 jana na JKT Ruvu inayofundishwa na mzalendo, Freddy Felix Minziro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao wa Bara kupoteza baada ya mechi 38 ndani ya misimu miwili.
Bao lililovunja rekodi za Omog na Azam leo lilifungwa na shambuliaji Samuel Kamuntu dakika ya 44, akimalizia krosi ya Najim Magulu aliyepasiwa na Jabir Aziz.
Mshambuliaji huyo aliyeingia uwanjani dakika ya 10, kuchukua nafasi ya Iddi Mbaga aliyeumia mapema tu anaifanya JKT ishinde mara ya pili mfululizo katika Ligi Kuu msimu huu, baada ya Jumamosi iliyopita kuichapa Prisons 2-1 na sasa inafikisha pointi saba baada ya kufungwa mechi mbili, sare moja na kushinda mbili.
Azam FC inabaki na pointi zake 10, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC- maana yake mbio za ubingwa sasa zimepamba moto.
Tayari kocha mpya wa Yanga SC, Mbrazil hawezi kuivunja rekodi hiyo, kwania alipoteza mchezo wa kwanza tu wa Ligi Kuu kwa kufunhwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Kocha Mzambia wa Simba SC, ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo, kwani hajapoteza mechi hata mja kati ya tano hadi sasa, akitoa sare zote. Omog atasafiri na Azam FC Jumamosi ijayo hadi Uwanja wa Nangwanda, Mtwara kuwafuata Ndanda FC.
0 comments:
Post a Comment