Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint-Preux yuko fiti kwa asilimia 100 kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya timu yake, Azam FC dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara Jumamosi.
Nyota huyo aliyesajiliwa msimu huu, hajacheza mechi hata moja ya Ligi Kuu kutokana na kuwa majeruhi akisumbuliwa na maumivu ya nyama aliyoyapata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC, Septemba 14, mwaka huu.
Katika mchezo huo ambao Aaam FC ililala 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Mhaiti huyo alitolewa kipindi cha pili baada ya kuumia nyama na tangu hapo hajaonekana uwanjani.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari amesema kwamba Leonel amefanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo na yuko fiti kabisa kucheza Jumamosi Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ameendelea kukinoa kikosi chake baada ya kipigo cha mwishoni mwa wiki cha 1-0 kutoka kwa JKT Ruvu, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Hicho kilikuwa kipigo cha kwanza kwa Omog baada ya mechi 18 za Ligi Kuu tangu ajiunge na Azam FC Desemba mwaka jana, akirithi mikoba ya Muingereza, Stewart John Hall.
Aidha, kipigo hicho pia kilichotokana na bao la mshambuliaji Samuel Kamuntu dakika ya 44, akimalizia krosi ya Najim Magulu aliyepasiwa na Jabir Aziz, kinakuwa cha kwanza kwa mabingwa hao wa Bara kupoteza baada ya mechi 38 ndani ya misimu miwili Hadi sasa, Leonel ameichezea mechi tano tu Azam, akiifungia mabao mawili.

Leonel Saint-Preux yuko fiti kucheza dhidi ya Ndanda FC Jumamosi |

0 comments:
Post a Comment