KATIKA kutafuta suluhisho la tatizo la majeruhi, Manchester United imemchukua Tabibu wa kikosi cha kwanza wa Southampton, Matt Radcliffe.
Louis van Gaal ana majerui tisa kuelekea mechi ya Ligi Kuu ya England mwishoni mwa wiki dhidi ya Everton.
Radcliffe anapewa heshima ya mmoja wa matabibu wazuri wa wachezaji kwenye soka na mechi yake ya mwisho kabla ya kujiunga na United itakuwa ya ugenini ya Southampton Uwanja wa White Hart Lane Jumapili.
Tabibu wa kikosi cha kwanza Southampton, Matt Radcliffe (kulia) anatarajiwa kuhamia Manchester United
Tabibu huyo mzoefu anachukuliwa United wakati ambao inapambana kupunguza tatizo la majeruhi kwa wachezaji wake.
Majerugi Man United kwa sasa ni Michael Carrick (enka), Marouane Fellaini (enka), Phil Jones (nyama), Ashley Young (nyonga), Jonny Evans (enka), Chris Smalling (paja) na Ander Herrera (mbavu).
Radcliffe, atakuwa kwenye benchi wikiendi hii wakati Saints watakapoungana na kocha wao wa zamani, Mauricio Pochettino kabla ya kuanza kibaruwa kipya Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment