WINGA wa Manchester United, Angel di Maria Jumatano alikuwa Carrington kwa matibabu katika siku yake ya mapumziko, katika jitihada za kocha Louis van Gaal kuhakikisha mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi anakuwa fiti kwa ajili ya mechi na Chelsea Jumapili.
Di Maria — tegemeo la Van Gaal kwa sasa kati ya nyota aliosajili, alitolewa wakati United ikienda sare ya 2-2 na West Brom katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu, kabla ya kugundulika aliumia mguu.
Haijatolewa taarifa rasmi na klabu hiyo, lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa Carrington kufanyiwa Jumatano na vyanzo vinasema mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina yuko katika nafasi ya kucheza Jumapili Uwanja wa Old Trafford.
Chelsea inatarajiwa kusafiri hadi Manchester bila mfungaji wao tegemeo Diego Costa na mbadala wake, Loic Remy, wote ni majeruhi.
United, wakati huo huo itamkosa Nahodha wake, Wayne Rooney ambaye atakuwa anamalizia adhabu yake ya kadi iliyomfanya akose mechi tatu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya West Ham.
0 comments:
Post a Comment