KOCHA Luis Enrique bado anasuasua kufanya maamuzi mazito zaidi tangu aanze kazi Barcelona – kumuanzisha ua kutomuanzisha mshambuliaji Luis Suarez kesho dhidi ya Real Madrid, lakini amethibitisha atacheza japo kidogo.
Suarez amemaliza adhabu yake baada ya kumng'ata Mtaliano Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunua la El Clasico ya kesho unatarajiwa kuwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano tangu Julai.
Lakini kocha wa Barca amekataa kusema kama atamuanzisa au la, akisema; "Hapana, siwezi kucheza mechi hiyo leo,"amesema leo Enrique.
"Suarez atapata dakika za kucheza, lakini siwezi kusema kiasi gani,"amesema. "Hii ni nafasi kubwa kwake kujipambanua katika timu mpya. Dakika ngapi atapata, siwezi kusema,".
0 comments:
Post a Comment