Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIUNGO Jerry Santo ameondoka leo Oman kurejea kwao, Nairobi, Kenya baada ya mipango yake ya kusaka timu ya kuchezea nchini humo kukwama.
Santo alikwenda Oman pamoja na wachezaji wawili wa Tanzania, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na mshambuliaji Betram Mombeki kwa ajili ya kujiunga na Oman Club, lakini hata hivyo hawakupata nafasi.
Chuji na Mombeki waliamua kurejea Dar es Salaam baada tu ya kukwama Oman Club, lakini Santo aliyewahi kuchezea Simba SC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga, akaamua kubaki kutafuta nafasi sehemu nyingine.
Hata hivyo, Wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mtanzania, Said Maaskary amesema Santo amekwama na amerejea nyumbani kwao.
“Dirisha la usajili linafungwa leo huku Oman na kwa bahati mbaya, Jerry Santo hajapata timu, hivyo anarejea nyumbani kwao (Kenya). Baada ya kukwama Oman Club, nilimpeleka katika klabu nyingine mbili, alifanya vizuri katika mazoezi, ila hakusajiliwa,”amesema Maaskary.

Jerry Santo kulia akiwa na Salum Ezry nchini Oman |
Hata hivyo, Wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mtanzania, Said Maaskary amesema Santo amekwama na amerejea nyumbani kwao.
“Dirisha la usajili linafungwa leo huku Oman na kwa bahati mbaya, Jerry Santo hajapata timu, hivyo anarejea nyumbani kwao (Kenya). Baada ya kukwama Oman Club, nilimpeleka katika klabu nyingine mbili, alifanya vizuri katika mazoezi, ila hakusajiliwa,”amesema Maaskary.
0 comments:
Post a Comment