WINGA Angel di Maria yuko fiti kuichezea Manchester United dhidi ya Chelsea Jumapili.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 60 katika klabu hiyo alikuwa alipata maumivu ya mguu United ikitoa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion Jumatatu na kulikuwa kuna wasiwasi ataukosa mchezo huo mkubwa zaidi kwa msimu huu hadi sasa.
Aliwekewa barafu baada ya kutolewa dakika ya 76 Jumatatu, lakini ameweza mkufanya mazoezi kwa siku mbili zilizopita na yuko tayari kwa kipute na Chelsea keshokutwa.
0 comments:
Post a Comment