KIUNGO wa Newcastle, Cheick Tiote amesema kwamba anataka kuondoka klabu hiyo na amekiri amekuwa katika mawasiliano na Arsenal.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amedumu kwa miaka minne Tyneside na kumekuwa na mapendekezo ya kuongezewa mkataba mpya, lakini sasa mpango huo upo shakani.
Tiote amewaambia Waandishi wa Habari nchini kwao kwamba: "Nataka kuondoma. Nimedumu kwa miaka minne na Newcastle. Nafikiri nimefikia kikomo ambacho labda ni wakati mwafaka kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine,"amesema.
Cheick Tiote amesema anataka kuondoka Newcastle aka sake changamoto mpya na amekiri juu ya mawasiliano na Arsenal
"NitaeIekeza nguvu zangu katika mechi zijazo na tune itakuwaje kati ya sasa na Desemba. Ni kweli kulikuwa kuna mawasiliano na Arsenal na klabu ya Urusi. Ningependa kubaki England,".
0 comments:
Post a Comment