MSHAMBULIAJI Fernando Torres amefunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza kuanza AC Milan timu yake hiyo mpya ikitoa sare ya 2-2 na Empoli iliyopanda Serie A msimu huu.
Baada ya mabao ya mapema ya Lorenzo Tonelli na Manuel Pucciarelli, Torres akaifungia Milan kwa kichwa dakika ya 43 na mwanasoka wa kimataifa wa Japan, Keisuke Honda akasawazisha kwa shuti la mbali dakika ya 58.
Milan alipata nafasi ya kuifungia Milan bao la ushindi wakati Torres, aliyejiunga na timu hiyo mwezi uliopita kwa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea, alimsetia Jeremy Menez dakika ya 62, lakini Mfaransa huyo akagongesha mwamba.
0 comments:
Post a Comment