WAKATI Manchester United inasaka mabeki, uwezekano wa kumpata Gerard Pique ni mdogo kutokana na mpenzi wake, mwanamuziki, Shakira kumzuia kuhama Barcelona.
Mpenzi wa beki huyo wa Barcelona hataki kuhama Jiji la Catalan kwenda Manchester. Na mpango wowote wa uhamisho wake kwenda United utapata upinzani mkali kutoka kwa mlimbwende huyo.
Pique hafurahii kuwekwa benchi Nou Camp baada ya kusajiliwa Jeremy Mathieu.
Pique (kulia) na mpenzi wake Shakira walipohudhuria mechi ya Kombe la Dunia mpira wa kikapu, michuano ya FIBA mjini Barcelona mapema mwezi huu
Gerard Pique akishangilia baada ya kuifungia Barcelona dhidi ya Apoel katika Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita
Pique (katikati) wakati anasajiliwa Manchester United mwaka 2004 akiwa na Sir Alex Ferguson (kulia) na David Gill
Taarifa nchini Hispania zinasema Pique anaweza kurejea Old Trafford, ambako Louis van Gaal anataka mabeki. Lakini Pique alitulizwa na kocha wa Barca, Luis Enrique wiki hii.
Kiungo huyo wa zamani wa Nou Camp amesema: "Juhudi za Pique ni kubwa, namna anavyojitolea na kujituma. Tatizo lake la nyonga limeisha, yuko tayari kutusaidia.'
Lakini Pique hajaingia kwenye mawasiliano na United, ambako aliondoka kuhamia Barcelona mwaka 2008.
Pique anafahamika vizuri mbele ya kocha wa Old Trafford, Van Gaal tangu ana umri wa miaka 13, na Mholanzi huyo anafahamiana pia na babu wa beki huyo.
0 comments:
Post a Comment