// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RUUD GULLIT AMTOLEA UVIVU VAN GAAL, AMUAMBIA "UMEBORONGA USAJILI, HUIJUI S9OKA YA UINGEREZA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RUUD GULLIT AMTOLEA UVIVU VAN GAAL, AMUAMBIA "UMEBORONGA USAJILI, HUIJUI S9OKA YA UINGEREZA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 28, 2014

    RUUD GULLIT AMTOLEA UVIVU VAN GAAL, AMUAMBIA "UMEBORONGA USAJILI, HUIJUI S9OKA YA UINGEREZA"

    MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ruud Gullit ameanzisha vita ya maneno na kocha Louis van Gaal akibeza usajili wake aliofanya Manchester United, kwa kusema kwamba umeonyesha kwamba haijui Ligi Kuu ya England kwa kujaza washambuliaji.
    Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Mwanasoka Bora wa Mwaka Ulaya, awali alikuwa anamuunga mkono van Gaal, hususan wakati wa Kombe la Dunia alipotetea mbinu zake katika timu ya taifa ya Uholanzi wakati van Gaal alipokuwa akikandiwa na magwiji kama Johan Cruyff.
    Lakini Gullit hajafurahishwa na usajili alioufanya Van Gaal Manchester United, akisaini wachezaji kama Angel Di Maria, Radamel Falcao, Ander Herrera, Luke Shaw, Daley Blind na Marcos Rojo wote wakigharimu Pauni Milioni 170, huku akipuuza kusajili mabeki.

    Ruud Gullit amesema Van Gaal amefanya makos a kusajili washambuliaji zaidi kuliko mabaki

    Na mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan anafikiri kwamba van Gaal ameweka imani kubwa kwa safu ya ushambuliaji ambayo ni utamaduni wa Kiholanzi, na akashindwa kuielewa Ligi Kuu ya England.
    Gullit amesema: "Inawezekanaje katika dunia hii kocha mzoefu na mwenye mafanikio anaweza kuanza msimu Man United bila kununua mabeki kadhaa halisi? Bado nastaajabishwa na usajili na uhamisho wake. Kama utaimarisha safu ya kiungo na ushambuliaji pekee kisha ukadharau nguvu ya timu nyingine za Ligi Kuu. 
    Kama unataka kufurukuta katika mashindano makubwa kwenye soka ya England uanze na kujenga msingi na kisha baadaye ujenge paa la nyumba yako. Van Gaal amefanya kinyume ya hivi.
    "Baada ya kuondoka kwa akina Nemanja Vidic kwenda Inter, na Rio Ferdinand kwenda QPR ilikuwa kawaida kwamba mabeki wapya wa kati walihitajika. Na alikuwa ana Pauni Milioni 200 za kutumia kwenye akaunti yake ya usajili. Ikiwa hautatumia sehemu ya fedha hizo kununua mabeki wazuri na wazoefu wa kati, basi huijui Ligi Kuu ya England,"amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUUD GULLIT AMTOLEA UVIVU VAN GAAL, AMUAMBIA "UMEBORONGA USAJILI, HUIJUI S9OKA YA UINGEREZA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top