NYOTA wa zamani wa Asrenal, Mfaransa Robert Pires amepata mapokezi makubwa wakati anawasili kwa ajili ya kusiani FC Goa ya India.
Pires alilazimika kusimama na kupiga picha na mashabiki na kuwasainia autographs wakati anawasili India na kisha akatweet: "Sikujua kama nina mashabiki wengi namna hii India!'
FC Go na mashabiki wa Arsenal wakimsubiri nyota huyo wa zamani wa Arsenal na Villarreal
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 40 amesitisha ustaafu wake kwenye soka na kurejea uwanjani kujiunga na FC Goa, moja ya timu nane katika Ligi iliyoundwa upya India na ataungana na nyota kadhaa waliowika Ulaya.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa Gunners, Freddie Ljungberg atachezea Mumbai City wakati Alessandro Del Piero, David Trezeguet, Elano, Mikael Silvestre na David James nao pia watacheza ligi hiyo.
Pires alistaafu mwaka 2011 wakati Mkataba wake na Aston Villa ulipomalizika, ambako alichukuliwa na Mfaransa mwenzake, kocha Gerard Houllier lakini akacheza mechi tisa tu klabu hiyo ya Midlands.
Wakati huo huo, beki wa zamani wa Inter Milan, Marco Materazzi amejiunga na Chennaiyin FC. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia anaweza pia kuwa mchezaji mbali ya kuwa kocha.
"Mimi ni kocha Mkuu," Materazzi ameliambia gazeti la The Hindu. "Wachezaji wetu watakuwa Elano, (Mikael) Silvestre na wengine wachezaji wa India. Tutasajili wachezaji wa kigeni watano au sita tu. "Hivyo, labda nitakuwa katika benchi. Na, hatuwezi kucheza bila wachezaji wa India. Tupo hapa kwa ajili yao,"amesema.
0 comments:
Post a Comment