IDARA ya Uhamiaji Tanzania imempa kibali cha muda mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ili achezee Simba SC na maana yake ataichezea klabu hiyo jioni ya leo dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali, Uhamiaji ilitoa vibali vya kufanyia kazi kwa wachezaji wawili wa Simba SC, Mrundi Pierre Kwizera na Mkenya Paul Kiongera pamoja na kocha wao, Patrick Phiri, lakini haikutoa cha Okwi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY mchama huu kwamba, baada ya kufuatilia wamegundua Okwi tayari alikuwa ana kibali kingine cha kufanya kazi Yanga SC.
“Kwa hiyo tumefanikiwa kupata kibali cha muda kwanza, baada ya leo tutafanya utaratibu wa kuwasiliana na ndugu zetu Yanga SC, ili waandike barua ya kwamba Okwi si mfanyakazi wao tena, ili sisi tuweze kupatiwa kibali chake kamili,”amesema Poppe.

Okwi amepata kibali cha kufanyia kazi Simba SC |
“Kwa hiyo tumefanikiwa kupata kibali cha muda kwanza, baada ya leo tutafanya utaratibu wa kuwasiliana na ndugu zetu Yanga SC, ili waandike barua ya kwamba Okwi si mfanyakazi wao tena, ili sisi tuweze kupatiwa kibali chake kamili,”amesema Poppe.
0 comments:
Post a Comment