// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA ATIMIZA MECHI 70 YANGA SC AKIFUNGA BAO LA 15 TANGU ATUE JANGWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA ATIMIZA MECHI 70 YANGA SC AKIFUNGA BAO LA 15 TANGU ATUE JANGWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 29, 2014

    MSUVA ATIMIZA MECHI 70 YANGA SC AKIFUNGA BAO LA 15 TANGU ATUE JANGWANI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WINGA Simon Msuva jana ametimiza mechi 70 za kuichezea Yanga SC tangu ajiunge nayo mwaka 2012 akitokea Moro United, tena akifunga bao la 15 kwa wana Jangwani hao.
    Msuva aliifungia Yanga SC bao muhimu la ushindi kipindi cha pili, mabingwa hao wa zamani wakishinda 2-1 mbele ya Prisons ya Mbeya na kuweka hai matumaini ya kutwaa tena taji la Ligi Kuu.
    Katika mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga walitangulia kupata bao dakika ya 34 mfungaji Andrey Coutinho kabla ya Prisons kusawazisha dakika ya 67 kupitia kwa Ibrahim Kahaka, kabla ya Msuva kufunga la ushindi dakika ya 69.  
    Simon Msuva akimtoka beki wa Prisons jana Uwanja wa Taifa katika mechi yake ya 70 na Yanga SC

    Katika mechi hizo 70 ambazo Msuva ameichezea Yanga SC, ndani yake kuna mataji manne, ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Kagame (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) na Ngao ya Jamii mara mbili.
    Kwa sasa, Msuva ndiye winga mkali zaidi katika soka ya Tanzania ambaye siku za karibuni ametokea kuwa tegemeo haswa la timu yake.
    Tangu kuwasili kwa kocha Mbrazil, Marcio Maximo amebadilisha matumizi ya mchezaji huyo na sasa anamtolea benchi kipindi cha pili kuja kuongeza kasi ya mchezo- na kweli huwa mwiba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA ATIMIZA MECHI 70 YANGA SC AKIFUNGA BAO LA 15 TANGU ATUE JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top