// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YASAKA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NGUVU KUZIBA PENGO LA KUKOSA MICHUANO YA ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YASAKA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NGUVU KUZIBA PENGO LA KUKOSA MICHUANO YA ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 29, 2014

    MAN UNITED YASAKA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NGUVU KUZIBA PENGO LA KUKOSA MICHUANO YA ULAYA

    KLABU ya Manchester United intake kucheza mechi za kirafiki za nguvu kuziba pengo la kukosa michuano ya Ulaya msimu huu na baada ya kutolewa katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup.
    Mabingwa wa rekodi Ligi Kuu England, mara 20 pato lao limepungua kwa asilimia 10 msimu wa 2014-2015 baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha David Moyes.
    Msoto huo umeifanya United ibaki na mechi moja tu ya katikati ya wiki kabla ya kumaliza mwaka 2014, na mechi tatu jumla katika miezi mitatu ya mwanzoni mwaka 2015.

    Usajili wa Angel di Maria na Falcao Manchester United unaweza kusaidia kupatikana kwa mechi za kirafiki za maana

    MECHI ZA MAN UNITED MWAKA HUU

    Manchester United haitakuwa na mechi ya katikati ya wiki hadi mwanzoni mwa Desemba
    Everton (nyumbani) Jumapili ya Oktoba 5
    West Brom (ugenini) Jumatatu ya Oktoba 20
    Chelsea (nyumbani) Jumapili ya Oktoba 26
    Man City (ugenini) Jumapili ya Novemba 2 
    C Palace (nyumbani) Jumamosi ya Novemba 8
    Arsenal (ugenini) Jumamosi ya Novemba 22
    Hull (nyumbani) Jumamosi ya Novemba 29
    Stoke (nyumbani) Jumanne ya Desemba 2
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YASAKA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NGUVU KUZIBA PENGO LA KUKOSA MICHUANO YA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top