BEKI Jonny Evans anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kuumia kifundo cha mguu Manchester United ikichapwa mabao 5-3 na Leicester City Jumapili.
Evans, ambaye ana historia ya maumivu ya enka na alihitaji upasuaji miaka miwili iliyopita, bado anataabika na tatizo hilo baada ya kuumia kipindi cha kwanza Uwanja wa King Power.
Beki huyo Ireland Kaskaini alifanyiwa vipimo Jumatatu na majibu ya awali yanaonyesha atakuwa nje kwa wiki nne.
Huku Phil Jones akipona maumivu ya nyama na Tyler Blackett anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Leicester, kocha Louis van Gaal anaumiza kichwa juu ya safu yake ulinzi kuelekea mechi na West Ham Jumamosi Uwanja wa Old Trafford.
Van Gaal tayari amemuarifu beki wa kushoto wa England, Luke Shaw kuanza kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 27 kutoka Southampton, na Marcos Rojo anatarajiwa kushirikiana na Chris Smalling katika beki ya kati.
0 comments:
Post a Comment