// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIVERPOOL YABANWA 2-2 NA BORO KOMBE LA LIGI, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIVERPOOL YABANWA 2-2 NA BORO KOMBE LA LIGI, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, September 24, 2014

    LIVERPOOL YABANWA 2-2 NA BORO KOMBE LA LIGI, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD

    KLABU ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.
    Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.
    Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90. 
    Mario Balotelli akipambana jana Anfield 
    Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao jana
    Suso akafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure akacheza rafu ndani ya boksi  na Patrick Bamford akaenda kusawazisha dakika za lala salama na katika penalty Liverpool ikashinda 14-13 baada ya Albert Adomah kupoteza mkwaju wa Boro.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Toure, Sakho, Enrique, Rossiter/Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana, Markovic na Lambert/Balotelli dk74.
    Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala, Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter, Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YABANWA 2-2 NA BORO KOMBE LA LIGI, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top