KIUNGO Frank Lampard anaweza akarejea Uwanja wa Stamford Bridge mwezi Januari, mwakani na kikosi cha Manchester City baada ya kugundulika kwamba muda wake wa kupiga kazi Etihad umeongezwa.
Lampard, ambaye amekuwa gwiji wa Chelsea baada ya kuitumikia kwa miaka 13, alikaribia kumwaga machozi baada ya kutokea benchi Jumapili na kuifungia City bao la kusawazisha katika sare ya 1-1.
Kufuatia kuonyesha kiwango kizuri kwa ujumla kwenye mchezo huo na hata mazoezini, City sasa wanataka kumuongezea mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 muda wa mkataba wake wa mkopo kutoka New York City FC ya Marekani waliomsajili baada ya kutemwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita.
Sasa huenda Lampard akaichezea City dhidi ya Chelsea Januari 31 mwakani, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kurejea Stamford Bridge tangu aondoke mwishoni mwa msimu kuelekea New York City FC.
0 comments:
Post a Comment