KOCHA Brendan Rodgers amesema uchezaji wa Liverpool umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na muundo mpya wa kikosi msimu huu.
Kocha huyo wa Liverpool, ambaye anaamini ushindi katika mechi ya mahasimu wa Merseyside kesho utaanzisha rasmi mbio za ubingwa msimu huu, amesajili wachezaji wapya tisa katika dirisha la msimu huu, huku akimpoteza kinara wake wa mabao, Luis Suarez aliyeuzwa Barcelona kwa Pauni Milioni 75.
Dalili hizo za kipindi cha mpito walichonacho Liverpool zimesababisha timu hiyo ipoteze mechi tatu kati ya tano za mwanzoni katika msimu huu wa Ligi Kuu England huku safu yao ya ulinzi ikionekana kuathirika, na Rodgers anakubali kiwango cha timu kwa ujumla kimeshuka kutoka msimu uliopita.
Kipindi cha mpito; Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anakiri yuko katika kipindi kigumu cha mopigo baada ya kuunda upya kikosi chake
Mario Balotelli amenunuliwa kuziba nafasi ya Suarez, nyota wa Uruguay aliyehamia Barca, lakini atahitaji muda kuwa sawa.
Hiyo ndiyo sababu anaamini Liverpool inahitaji kurudi katika misingi ambayo iliwasaidia msimu uliopita na amekuwa akiridhishwa na namna ambavyo kikosi chake kinajifunza kutokana na makosa.
"Nafikiri hadi sasa tunapaswa kuelekeza fikra zetu na kuingiza mbinu mbadala katika mechi zetu ambayo ilitupa wimbi la ushindi miezi 18 iliyopita,"amesema Rodgers.
Liverpool imepoteza mechi tatu kati ya tano za mwanzoni za Ligi Kuu na sasa inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo
Liverpool inamkosa mshambuliaji wake Luis Suarez ambaye mabao yake yameirejesha timu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu
0 comments:
Post a Comment