• HABARI MPYA

        Sunday, September 21, 2014

        JIMMY CHIZI ATOA BONGE LA WIMBO AKIMSHIRIKISHA KHALID CHOKORA

        Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
        MSANII James Lutufyo, maarufu kama Jimmy Chizi ametoa wimbo wake uitwao Sheila ambao amemshirikisha Khalid Chokora.
        Jimmy ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wimbo huo amerekodi katika studio za Amoroso Sound mjini Dar es Salaam na ameuita; ‘Babu kubwa’. Amesema amerekodi wimbo huo katika mtindo wa Afrikan na amesema; “umebamba ile mbaya”. Kuhusu video, Jimmy aliyeibuka pamoja na Papi ‘Kocha’ Nguza kimuziki ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha jela, amesema; “Video inakuja, na itakuwa video moja simpo, lakini yenye akili sana, watu wangu wakae mkao wa kula”.
        Jimmy Chizi kushoto ametoa wimbo mkali unaitwa Sheila

        Amesema tayari wimbo huo umekwishasambaza kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini kote na harakati za kuusambaza kimataifa zaidi zinafuatia.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: JIMMY CHIZI ATOA BONGE LA WIMBO AKIMSHIRIKISHA KHALID CHOKORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry