MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu yake Paris Saint-Germain dhidi ya Barcelona kesho kutokana na maumivu ya kisigino.
Mabingwa hao wa Ufaranwa wametangaza leo kwamba nyota huyo wa Sweden, ambaye amekosa mechi mbili zilizopita za Ligue 1, hajapona sawia maumivu yake ya kisigino na ataikosa mechi hiyo dhidi ya timu yake ya zamani.
PSG iliufanyia vipimo mguu wa mpachika mabao huyo leo, lakini imeonyesha haujapona sawasawa kuweza kucheza dhidi ya Barca.
Zlatan Ibrahimovic ataikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa baina ya PSG na Barcelona sababu ya maumivu ya kisigino
Mshambuliaji huyo wa Sweden tayari amekosa mechi mbili na hayuko fiti kiasi cha kutosha kucheza dhidi ya Barcelona
Mara ya mwisho Ibrahimovic kuichezea PSG ilikuwa Septemba 21 katika sare ya 1-1 nyumbani na Lyon na tangu halo amekosa mechi ambazo timu yake ilishinda 2-0 dhidi ya Caen na kutoka sare ya 1-1 na Toulouse.
Paris ilivuna pointi moja katika mechi ya kwanza ya Kundi F ugenini dhidi ya Ajax wakati wapinzani wao, Barcelona waliifunga APOEL Nicosia 1-0.
Ibrahimovic alikuwa Barca msimu wa 2009-2010 ambako alifunga mabao 21 katika mechi 45 lakini hakumvutia kocha wa timu hiyo wakati huo, Pep Guardiola na akahamia AC Milan.
Wasiwasi ni kwamba, kwa PSG, wameshinda asilimia 40 tu ya mechi ambazo walimkosa brahimovic uwanjani. Tayari timu hiyo ya Ufaransa inamkosa nyota wake mwingine, Ezequiel Lavezzi, ambaye aliumia nyama katika mechi na Caen na atakuwa nje kwa wiki tatu.
0 comments:
Post a Comment