MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge amewataja Thierry Henry, Ronaldo na Robbie Fowler miongoni mwa wakali wa mabao waliomvutia wakati anaibuka akiwa mdogo.
Mkali huyo wa mabao wa Wekundu wa Anfield na England ameandika kwenye Instagram jana na kuweka kuweka picha za watatu wote hao miongoni mwa washambuliaji sita mashujaa wake.
Orodha yake inakamilishwa na wakali kama akina Dennis Bergkamp, Tino Asprilla, Rivaldo, Gianfranco Zola, Ian Wright na Nicolas Anelka.
Mashujaa wa Sturridge wakiwemo Robbie Fowler, Dennis Bergkamp, Tino Asprilla, Henry juu kulia na mshindi wa Kombe la Dunia 1994 na 2002 akiwa na Brazil Ronaldo (chini kulia)
Amembatanisha maelezo kwenye picha hiyo kwamba; "Wakali naowazimia muda mrefu...Fowler, Bergkamp, Asprilla, Ronaldo, Henry, Rivaldo, Zola, Wright, Anelka...'
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anatumai kuvunja rekodi ya gwiji wa Kop, Fowler alipokuwa Anfield, ambaye alifunga mabao 183 katika mechi 369 games, baada ya mwanzo mzuri katika miezi yake 20 katika klabu hiyo.
Sturridge amefunga mabao 36 katika mechi 52 alizocheza Liverpool, na kwa sasa anapambana kupona maumivu aliyoyapata mapema mwezi huu akiwa na timu ya taifa, ili arejee uwanjani.
0 comments:
Post a Comment