KIUNGO Jack Wilshere amerejea mazoezini Arsenal leo asubuhi baada ya kupona maumivu aliyoyapata wiki iliyopita.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa kwenye janga la viungo wake kuuima kwa Aaron Ramsey, Mikel Arteta na Wilshere wote kuumia kwenye mechi na Tottenham Jumamosi.
Wilshere aliumia enka na kulikuwa kuna wasiwasi amepata madhara makubwa katika sehemu ambayo imekuwa tatizo la muda mrefu kwake.
Wenger amesema: "Jack Wilshere yuko kikosini kwa ajili ya mechi ya kesho, tutamuanzisha? bado sijajua, lakini yuko kikosini.
"Tuliwapoteza Mikel Arteta na Aaron Ramsey kwenye mechi yetu iliyopita na wangekuwa watatu, kwa sababu Wilshere alikuwa shakani kwa muda mrefu, lakini amepona haraka,".
Theo Walcott (kulia) akitembea na Serge Gnabry kuelekea mazoezini leo
Lakini kiungo huyo wa England amerejea na kuonekana akiwa vizuri wakati akifanya mazoezi na Arsenal viwanja vya mazoezi vya timu hiyo, Colney.
Wilshere alikuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi mazoezini leo akipigiana mipira na Alexis Sanchez, Mathieu Flamini na Francis Coquelin.
Kisha kikosi cha wachezaji 18 kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray kikaanza kukimbizwa na kocha wa mazoezi ya nguvu Shad Forsythe, Mmarekani aliyechukuliwa kutoka kikosi cha Ujerumani kilichotwaa Kombe la Dunia.
Theo Walcott aliibuka baadaye zaidi ya wachezaji wengine wote na kufanya mazoezi mepesi peke yake akijiandaa kurejea uwanjani, baada ya winga huyo kukosekana tangu Januari 4, alipoumia dhidi ya Tottenham kwenye Kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment