KLABU ya Manchester United imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Mpachika mabao huyo ataigharimu klabu hiyo ya Old Trafford Pauni Milioni 12 kwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo katika orodha ya wachezaji wapya kwenye kikosi cha Louis van Gaal.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 tayari ameafiki kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na anatarajiwa kutua Manchester wakati wowote kwa ndege binafasi kukamilisha taratibu.
0 comments:
Post a Comment