BEKI Daniel Agger amerejea klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 baada ya Mdenmark huyokukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 3 kujiunga na Brondby.
Mlinzi huyo wa kati mwenye umri wa miaka anakwenda klabu hiyo ya Denmark kwa Pauni Milioni 3 baada ya kupiga kazi Anfield kwa miaka nane.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Denmark amecheza jumla ya mechi 232 klabu hiyo ya Merseyside, lakini ametwaa taji moja tu, Kombe la Ligi mwaka 2012, maarufu kama Carling Cup Uwanja wa Wembley.
0 comments:
Post a Comment