// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BILA RONALDO, REAL MADRID YAPIGWA 4-2 LA LIGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BILA RONALDO, REAL MADRID YAPIGWA 4-2 LA LIGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 01, 2014

    BILA RONALDO, REAL MADRID YAPIGWA 4-2 LA LIGA

    REAL Mdrid jana imefumuliwa mabao 4-2 na Real Sociedad katika mchezo w La LIga Uwanja wa San Sebastian.
    Kocha wa Real, Carlo Ancelotti alimkosa Cristiano Ronaldo, ambaye alimpumzisha hivyo kuwategemea Gareth Bale, James Rodriguez na wenzake.
    Sergio Ramos aliifungia Real bao la kwanza dakika ya sita, kabla ya Bale kufunga la pili dakika ya 11, lakini wenyeji wakatoka nyuma na kushinda 4-2 wakimtungua Iker Casillas.
    Sergio Ramos akiugulia maumivu katika mchezo wa jana

    Mabao ya Inigo Martinez dakika ya 36, Carlos Vela aliyetokea benchi dakika ya 76 na David Zurutuza mawili dakika za 41 na 65 yalitosha kuirdisha Real mikono mitupu mjini Madrid.
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Carvajal/Arbeloa dk77, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric/Khedira dk74, Kroos, Isco, Bale, Benzema na Rodriguez.
    Real Sociedad: Zubikarai, Zaldua, Elustondo, I Martinez, De La Bella, Bergara, Granero, Prieto/Gonzalez dk83, Zurutuza, Castro/Canales dk59 na Agirretxe/Vela dk59.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BILA RONALDO, REAL MADRID YAPIGWA 4-2 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top