KOCHA wa Barcelona, Luis Enrique atawapiga faini Lionel Messi na mchezaji mwingine yeyote wa timu hiyo hadi Pauni 1,200 kwa mechi iwapo watachelewa kuwasili hata dakika moja siku ya mchezo.
Mwalimu huyo wa Barca anaamini nidhamu ni funguo wa mafanikio katika harakati za ubingwa wa La Liga, na Enrique hatamuonea aibu mchezaji yeyote Nou Camp.
Kuchelewa katika mechi ya Barcelona itashuhudhiwa Enrique akimkata mchezaji pauni 300, kabla dau halijapanda mara mbili hadi Pauni 600 na Pauni 1,200 akirudia mara ya pili na ya tatu.
Faini zitapigwa pia katika kuchelewa mazoezi, vikao na kwenye miadi. Haya yote yanakumbushwa wakati Barca ikilazimishwa sare ya 0-0 na Magala jana katika La Liga.
0 comments:
Post a Comment