KUREJEA Ligi Kuu ya England pekee ni kama hakukutosha kwa Mario Balloted kuwavutia watu na sasa mshambuliaji huyo ameamua kubadilisha na mtindo wa nywele zake.
Wekundu wa Anfield walimsajili Balotelli kutoka AC Milan kwa Pauni Milioni 16 msimu huu, na kocha Brendan Rodgers amemtaka Mtaliano huyo kutuliza kichwa na kufunga mabao.
Na wakati Rodgers akissistiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 si mtata, anaibuka na mtindo mpya wa nywele ambao utazua gumzo.
Moja ya mitindo ya nywele ya Balotelli wakati anachezea Manchester City kama anavyoonekana hapa wakati akidhibitiwa asigombane na Joey Barton mwaka 2012
Huu ni mtindo wa nywele alioingia Liverpool Balotelli kama anavyoonekana hapa akifunga penalti dhidi ya Middlesbrough juzi katika mechi ya Kombe la Ligi
0 comments:
Post a Comment