KIUNGO Ander Herrera anatarajiwa kuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kuchanika mbavu akiichezea Manchester United dhidi ya West Ham Jumamosi.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alimpisha Antonio Valencia baada ya kuumia katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Taarifa iliyotolewa na United leo mchana imesema: "Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera amechanika mbavu wakati wa mechi na West Ham United Jumamosi.
"Mspanyola huyo alitolewa dakika ya 74 na klabu hiyo itaendelea kuangalia hali yake kwa karibu katika wiki kadhaa,".
Herrera anakuwa mchezaji wa tisa wa kikosi cha kwanza cha Louis van Gaal kuwa nje ya Uwanja kwa sababu ya maumivu na wengine wakitumikia adhabu wakati inajiandaa na mechi dhidi ya Everton Jumapili.
Haifahamiki ni muda gani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atakuwa nje kwa maumivu hayo, ambayo ni pigo lingine kwa kocha wake.
Herrera amekuwa katika kiwango kizuri United tangu ajiunge nayo kutoka Athletic Bilbao mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Amecheza mechi za Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City, Queens Park Rangers, Leicester City na West Ham.
Alifunga bao la pili la United katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR na akaifanya United ionize 3-1 mbele ya Leicester, kabla ya kufungwa 5-3.
0 comments:
Post a Comment