KIZAZI kijacho cha Ujerumani kinafuata vyema nyayo za kaka zao baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa cijana chini ya umri wa miaka 19.
Kiungo wa Hertha Berlin, Hany Mukhtar alifunga bao pekee dakika ya 39 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ureno mjini Budapest.
Hiyo inafuatia kaka zao, timu ya wakubwa ya Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia baada ya kuifunga Argentina nchini Brazil mapema mwezi huu.
Kifaa: Mukhtar akifunga bao pekee lililoipa Ujerumani ubingwa wa U19
Julian Brandt akiwatoka mabeki watatu wa Ureno
0 comments:
Post a Comment