MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu yake JS Kabylie imesema.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na kitu hicho kigumu mwishoni mwa mchezo kati ya JS Kabylie na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Taarifa katika tovuti ya Kabylie jana imesema: "Wizara ya Mambo ya Ndani na Serikali ya Nyumbani, kupitia Waziri Tayeb Belaiz, imeagiza uchunguzi wa wazi uanze mara moja juu ya tukio hilo lililosababisha kifo cha Albert Ebosse.
Majanga: Mshambuliaji wa Cameroon, Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kigumu kichwani kilichorushwa kutoka jukwaani
Ebosse aliifungia bao Kabylie katika mechi hiyo iliyoisha kwa kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa USM Alger.
0 comments:
Post a Comment