KLABU ya Tottenham imekamilisha usajili wa mwanasoka wa kimataifa wa Marekani, DeAndre Yedlin kwa Mkataba wa miaka minne.
Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 21, atabaki Seattle Sounders kabla ya kujiunga na kikosi cha Mauricio Pochettino msimu wa 2015/2016.
Akizungumza na tovuto ya klabu hiyo, Yedlin alisema; "Nimefurahishwa sana kuja Ligi Kuu ya England na kujishindanisha dhidi ya baadhi ya wachezaji bora duniani,".
0 comments:
Post a Comment