KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuogelea katika bwawa la maji moto Manchester United, baada ya usiku huu kfungwa na Mk Dons ya Daraja la Kwanza mabao 4-0 katika michuano ya Kombe la Ligi, maarufu Capital One.
Mabao yaliyomtia machungu Van Gaal leo yamefungwa na Will Grigg dakika ya 25 na 63 na Benik Afobe anayecheza kwa mkopo kutoka Arsenal dakika ya 70 na 83.
Kocha Msaidizi Ryan Giggs alionekana kufuta machozi baada ya bao la tatu, akiwa kwenye benchi na bosi wake, van Gaal.
Kikosi cha MK Dons: Martin, Baldock, McFadzean, Kay, Lewington, Alli, Potter, Carruthers/Green dk61, Reeves, Bowditch/Powell dk56 na Grigg/Afobe dk68.
Manchester United: De Gea, M.Keane, Evans, Vermijl 5, Janko/Perrara dk46, Anderson, Kagawa/Januzaj dk20, Powell/Wilson dk57, James, Hernandez na Welbeck.
Manchester United: De Gea, M.Keane, Evans, Vermijl 5, Janko/Perrara dk46, Anderson, Kagawa/Januzaj dk20, Powell/Wilson dk57, James, Hernandez na Welbeck.
Wachezaji wa United wakiwa hoi baada ya kipigo
Wachezaji wa MK Dons wakishangilia bao lao la kwanza
Grigg akimtungua kipa De Gea
0 comments:
Post a Comment