// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 24, 2014

    MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI

    KOCHA Louis Van Gaal kwa mara nyingine ameshindwa kuipa ushindi Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland Uwanja wa Light katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 
    Juan Mata alitangulia kuifungia United dakika ya 17, lakini Jack Rodwell akaisawazishia Black Cats dakika ya 30. Robin van Persie alirejea kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu leo kwa mara ya kwanza tangu baada ya Kombe la Dunia, lakini akashindwa kuibeba timu hiyo.
    Hali tete; Wachezaji wa Manchester United, kutoka kulia Wayne Rooney, Juan Mata na Robin van Persie wakiwa hawaamini macho yao baada ya Sunderland kusawazisha bao

    Kikosi cha Sunderland kilikuwa; Mannone, Vergini, O'Shea, Brown, Van Aanholt, Larsson, Cattermole, Rodwell/Gomez dk63, Buckley/Bridcutt dk79, Fletcher/Altidore dk76 na Wickham. 
    Manchester United: De Gea, Jones, Smalling/Michael Keane dk44, Blackett, Valencia, Fletcher/Januzaj dk64, Cleverley, Young, Mata, Van Persie/Welbeck dk64 na Rooney. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top